Saturday 1 March 2014

KIZUNGUMKUTI CHA UGATUZI!

Mengi yamesemwa kufuatia miswada miwili katika Mbunge ya Seneti, inayowalenga magavana na kwa lugha ya mtaani, ‘kuwatia adabu’. Lakini je, kunayo mengi ambayo wabunge na masenei hawawaambii wakenya?
Baada ya Gavana wa Kaunti ya Embu, Martin Wambora kutimuliwa mamlakani,vita hivi vimechukua mwelekeo mpya. Magavana wamekataa kufika mbele ya tume hii licha ya kutakiwa kufanya hivyo na ata kunena ya kwamba hawawajibiki kwa mbunge ya Seneti, mbali kwa mbunge za kaunti. Kwa upande mwingine, maseneti na wabunge wameahidi kuwatia adabu kwa kupitisha miswada ya:
                    :kuyaondoa mataji ya His Excellency,
                    :Kutopeperusha bendera ya taifa kwenye magari yao ya shughuli za kirasmi
                     kama magavana, kati ya mengine mengi. Swali ni je, haya yote ni uwajibikaji wa kikazi na kwa majukumu yao kikatiba?
Huku maseneta wakijitayarisha kujadili miswada hii, na kulingana na jinsi mambo yalivyo, kuipitisha, kama taifa na watu wake, tunafaa kujsahilii kimoyo, kuyawaza na kuamua kuhusu yote haya yanayofanyika katika ulingo wa kisiasa. Kunao mvutano baina ya magavana, maseneta na wabunge. Mbunge zetu katika kaunti zote 47, magavana na maseneta wanaomajukumu  makubwa kikatiba na kimaadili, ya kutekeleza, mbali sio kupigana vita visivyomfaidi mkenya wa kawaida.
Yafaa tujenge na kuinua kaunti zetu kupitia ugatuzi, jinsi ambavyo Gavana wa Machakos, Dkt. Alfred Mutua anafanya. Tusigatue ufisadi na uporaji wa mali ya uma kwa kisingisio cha kuuendeleza na kutetea ugatuzi.
Ugatuzi ni Baraka kwa nchi yetu, haswa katika maeneo ambayo yametengwa na kubakia nyuma kimaendeleo, kama vile eneo ya Kaskazini mwa Kenya kati ya maeneo mengine. Lakini yafaa tujihadhari na uongozi mbaya na usiowajibika, ufisadi uliokithiri, uporaji wa mali uma na mali asili, na pia siasa sisizofaidi mkenya wa kawaida huko mashinani. Ugatuzi ni baraka ukitekelezwa kwa njia ifaayo, lakini pia ni laana iwapo utatumiwa vibaya.
Maswala ya usalama, muundo msingi, hospitali na sekta yote ya afya, Nyanja ya masomo, ukosefu wa maji, uhaba wa chakula cha kutosha na mengineyo mengi anayoitaji mkenya wa kawaida na nchi yote kwa jumla, ni maradhi ambayo tiba yake ni ugatuzi.
Tufuate sheria, maadili mema na wajibu wa kila mmoja kwa nchi na watu wake, ili ugatuzi ujenge Kenya na pia tuyaafikie malengo ya Ruwaza ya 2030. Sote tu ndugu wakenya na kaunti zote 47 zikinawiri, bila shaka Kenya yetu itasonga mbele!

No comments:

Post a Comment